Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imetoa msaada wa madawati mia moja na kumi yenye thamani ya shilingi kwa shule za msingi Sinde, Maanga, Lyoto na Ilomba ili kuboresha huduma za elimu kwa shule hizo.

Akikabidhi msaada huo wa madawati meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lukesia Bena amesema benki yake imetoa msaada huo baada ya kuridhia ombi lililotolewa na mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kwa benki hiyo kusaidia madawati kwa shule za msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi kupenda masomo.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Mbeya Afisa elimu wa shule za msingi jiji Bi.Aurelia Luensi ametoa shukrani kwa uongozi wa Benki hiyo kuchangia katika elimu na kuwasihi walimu na wanafunzi kuyatunza madawati hayo.

Naye mwakilishi wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ambaye ni diwani wa kata ya Sinde Fanuel Kuanula amesema misaada hiyo imefika kwa wakati muafaka ambapo wanafunzi wanauhitaji mkubwa wa madawati kutokana na yale yaliyopo kuchakaa.

Shule ya msingi Sinde imepata madawati 34, Lyoto 36, Ilomba 15 na Maanga 28.

Post a Comment

 
Top