Menu
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwake Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Shamba hilo ni la nyasi za kulishia mifugo kwa njia ya kisasa (zero grazing), akiwa ni mmoja wa wafugaji kijijini hapo. Rais Kikwete, ambaye aghalabu hutumia muda wake wa likizo shambani kwake, pia analima mananasi ambayo hustawi vizuri katika wilaya hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwantumu Mahiza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwako Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Shamba hilo ni la manyasi ya kulishia mifugo.
PICHA NA IKULU.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Longido ngombe watano na mbuzi katika sherehe ambayo jumla ya kaya 16 zilikabidhiwa ngombe na mbuzi baadaya kuathirika na janga la kiangazi ambapo baadhi wakazi wa wilaya za Longido,Ngorongoro na Monduli walipoteza mifugo yao yote. Katika zoezi hilo serikali imetoa jumla ya ngombe zaidi ya 25,000 na zaidi ya mbuzi 15,000 ili kuzisaidia familia hizo kuanza tena maisha yao yanayotegemea sana mifugo.Sherehe za makabidhiano hayo zimefanyika wilayani Longido, mkoani Arusha jana.
(picha na Freddy maro).

Post a Comment

 
Top