Menu
 

Waheshimiwa majaji  wanasheria na watumishi wa mahakama wakiangalia gwalide lililoandaliwa na jeshi la polisi mkoani mbeya.
*****
 Habari na Mwandishi wetu
Serikali imetakiwa kutoa elimu ya sheria na adhabu anayopewa mshtakiwa ili kuleta ushirikiano baina ya mahakama na jamii ili kuwajenga wananchi kuwa na imani na muhimili huo wa dola.

Rai hiyo imetolewa na Jaji mfawidhi Bethel Milla wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya mahakama kuu ya Tanzania iliyopo Forest jijini hapa.

Amesema Mahakama ni chombo chenye maamuzi ya mwisho katika Serikali yoyote duniani na kwamba jamii inatakiwa kuheshimu taratibu na kanuni zinazotolewa na mahakama.

Naye mwenyekiti wa wanasheria wa kujitegemea mkoani Mbeya Bwana Makolo amesema Sheria inamlinda mwanamke mjamzito kunyongwa na badala yake sheria hiyo inatoa adhabu ya kifungo cha maisha kwa mwanamke huyo ili kumnusuru mtoto anayemtarajia dhidi ya adhabu ya mama yake.

Maadhimisho ya siku ya sheria nchini huadhimishwa kila siku za mwanzo wa mwezi wa pili.

Post a Comment

 
Top