Menu
 

Wafanyabiashara wadogo wadogo wajulikanao kama wamachinga wakiwa wamepanga bidhaa zao katika kituo cha kidogo cha mabasi Ubungo kama unavyowaona mwenyewe, kwasasa biashara katika eneo hilo imeshamili sana mpaka wahusika wamejisahau kabisa sijui serikali inafanyaje kuhusu watu hawa???
Wafanyabiashara wengine walikuwa wanafanya minada
kila kitu kinapatikana hakuna haja ya kwenda sokoni ama kwenye maduka.

Hali ya Bara bara ya Morogoro Road eneo la Ubungo mataa lipo katika hali ya hatari sana, hasa kutokana na kasi ya wafanya biashara ndogo ndogo ,maarufu kama wamachinga wanavyoongezeka kwa kasi katika eneo hilo, ni jambo la kushangaza sana kuona hali hii inavyoachwa kana kwamba wahusika hawaioni (Serikali), tunapenda kuwahasa kwa mara nyingine tena Serikali jaribuni kuliangalia hili, wafanya biashara hawa wanafanya biashara katika mazingira ya hatari sana na yasiyo rasmi.(Kwa hisani ya swahilinawaswahili.blogspot.com)

Post a Comment

 
Top