Menu
 


Habari na Mwandishi wetu
Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi TUCTA mkoani Mbeya limepata viongozi wapya watakaoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Viongozi hao wamepatikana kufuatia uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Wafanyakazi kilichopo Mwanjelwa jijini Mbeya chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TUCTA bwana NICHOLOUS MGAYA.

Katika uchaguzi huo Alinanuswe Mwakapala ametetea nafasi yake na kuendelea kuwa mwenyekiti wa shirikisho hilo ngazi ya mkoa na Thomas Kasombe akachaguliwa kuwa katibu.

Mwakilishi wafanyakazi wanawake Peles Lugala, Mwakilishi wa vijana Nasra Nasoro na Willium Barton akachaguliwa kuwa mwakilishi wa wafanyakazi walio na ulemavu.

Awali katibu mkuu Mgaya aliwataka viongozi waliochaguliwa kutambua kuwa nafasi walizopewa zinatokana na kuaminiwa na wafanyakazi kuwa wanao uwezo wa kuwaongoza hivyo wana wajibu wa kuhakikisha wanajituma katikaa utendaji kazi wao.

Post a Comment

 
Top