Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wafanyabiashara kutoka mji mdogo wa Mlowo, wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya bado wameendelea na msimamo wao wa kugoma kulipa ushuru wa soko na mazao kwa halmashauri ya wilaya hiyo kutokana na mazimio yaliyofanywa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  siku ya alhamisi  Februari 16 mwaka huu katika mji huo.

Kukosekana kwa huduma za choo na kusanyiko wa takataka wa muda mrefu bila kuzolewani sababu zilizochangia wafanyabiashara hao kugoma kulipa ushuru, licha ya kuwepo kwa makusanyo ya kila siku kutoka kwa wafanyabiashara hao na ushuru hutozwa  kutokana na mazao yanayosafirishwa kutoka wilayani humo.

Kufatia mgomo huo uongozi wa wa halmashauri hiyo umeamua kuitisha kikao  cha dharula ili kupata mustakabali wa suala hili ambao limeendelea kuikosesha halmashauri ya wilaya ya Mbozi mapato yake yanayotokana na vyanzo hivyo.

Katika mkutano huo mkuu wa wilaya hiyo Mheshimiwa Gabrel Kimoro alialikwa kuhudhuria ambapo uchunguzi umebaini mara kadhaa amekuwa akialikwa na bila kuhudhuria, hali ambayo ilichangia kuwa moja ya ajenda ambapo wengi wamelalamikia katika mkutano huo uliohudhuriwa na wananchi zaidi ya mia nne wa mji wa Mlowo.

Wakati huo huo sakata la Shule ya msingi Ichenjezwa kukataa kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza imechukua sura mpya baada ya watoo watatu kuandikishwa darasa la pili na kuanza masomo huku watoto wengine wakikataliwa uchunguzi huo umebainiwa .

Post a Comment

 
Top