Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Wafanyabiashara wa soko la Bomba Mbili liliopo mtaa wa Shewa kata ya Ilomba wapo hatarini kukumbwa  na mlipuko wa magonjwa kutokana na ukosefu wa vyoo na sehem ya kutupia taka.

Akizungumza na Bomba Fm mmoja wa wafanyabiashara  BI Monica Ezekiel amesema wamekuwa wakifanya biashara kwa mda mrefu bila choo wala sehem ya kutupia taka hali iliyopelekea soko hilo kuwa na mazingira hatarishi kwa afya ya wanadamu.

 Kwa upande wake mwanyekiti wa soko hilo bwana Edson Kyomo amesema uongozi wa soko hilo upo mbioni kutenga eneo maalum la kutupa taka na kujenga vyoo ili kuepukana na magonjwa yanayoweza kujitokeza  kutokana na hali hiyo. 

Post a Comment

 
Top