Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Wananchi wa kata ya Sangambi wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wameanza ujenzi wa shule ya msingi katika kijiji cha Izumbi ili kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi.

Akiongea na mtandao huu Afisa mtendaji wa kata hiyo bwana Ongara Daudi amesema wameamua kujenga shule kijijini hapo kwa sababu wanafunzi wengi wamekuwa hawahudhurii masomo kwa sababu ya umbali wa shule iliyopo sasa

Aidha Daudi ameongeza kuwa wanakijiji wengi wamepata hamasa na kuonyesha juhudi ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo pia ameiomba serikali kuwaunga mkono wanakijiji ili kukamilisha malengo yao.

Hata hivyo amesema uhamasishaji wa ujenzi huo unalengo la kufuta ujinga kwa kizazi cha sasa na kijacho kujikomboa kielimu na kupunguza wimbi la idadi kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika wilayani humo.

Post a Comment

 
Top