Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Wakazi wa kata ya Itezi jijini Mbeya wamegoma kuchangia michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kutokana na kata hiyo kuwa na idadi kubwa ya vyumba vya madarasa ambavyo havitumiki.

Wakiongeaa katika mkutano baada ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama kufanya ziara ya kukagua maendeleo kwenye kata hiyo wakazi hao wamesema hawezi kuchanga michango kutokana na vyumba vilivyopo kutotumika kama ilivyokusudiwa na badala yake hutumika kufugia wanyama.

Mmoja wa wakazi wa kata hiyo amesema vyumba vilivyopo vinauwezo wa kuwachukuwa wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu lakini wamekuwa wakichangishwa michango wakati vyumba vilivyopo vikitumika kufugia mbuzi.

Akiongea na wananchi hao Mkuu wa wilaya ya Mbeya Evansi Balama amesema malalamiko hayo wameyasikia na yatafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na viongozi wa kata hiyo kuwajibishwa kwa kutumia ovyo vyumba vya madarasa.

Post a Comment

 
Top