Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Wanawake watatu wazee wa kijiji cha Usevya, wilayani Mpanda wameuawa na wananchi wakituhumiwa kuroga mvua isinyeshe.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, amewataja waliouawa kuwa ni Consolata Nsokilo mwenye umri wa miaka 64, Oliveta Pesambili mwenye umri wa miaka 74 na mwingine wa tatu jina lake halikuweza kupatikana mara moja.

Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa baada ya tukio hilo mvua kubwa ilinyesha kwa zaidi ya saa moja kuanzia saa nne asubuhi na kuibua hisia tofauti miongoni mwa wakazi wa Usevya.

Kabla ya mauji hayo wananchi wa kijiji hicho waliwalazimisha marehemu kuachia mvua kunyeesha na baada ya kuona kuwa mvua hainyeshi ndipo walipoanaza kuwashambulia marehemu hao kwa kutumia silaha za kijadi.

Kutokana na tukio hilo hadi sasa jeshi la polisi mkoani Rukwa limewashikilia watu kumi kwa kuhusika na mauji hayo na kwamba upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea.

Post a Comment

 
Top