Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kuingia nchiini bila kibali, kukutwa na kete za bangi na kumiliki silaha ambapo ni kinyume cha sheria.

Akizungumzia kutokea kwa matukio hayo Kaimu  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Barakiel Masaki  amesema kuwa katika tukio la kwanza lilitokea Februari 23, mwaka huu maeneo ya Uyole  jijini Mbeya, ambapo Polisi wakiwa doria walimkamata Bwana Fakaso Ugala (25) raia wa Ethiopia pamoja na wenzake watatu  kwa  kosa la kuingia nchini bila kibali.

Katika tukio jingine  lililotokea siku hiyo hiyo majira ya saa kumi jioni katika eneo ya Mlowo katika wilaya ya Mbozi mkoani hapa  Bwana Ezila Chilenga Mlamba (31) ambaye ni mfanyabiashara alikamatwa akiwa na bangi kete 815 ambazo ni sawa na kilo 1 na gramu 125 akiwa ameficha katika kibanda chake cha biashara.

Hata hivyo tukio la mwisho lilitokea majira ya saba mchana katika kijiji cha Ipande katika wilaya ya Kyela Atambwile Mwakalukwa  (25) na Dankeni Mwakalukwa (40)  wote wakazi wa Kijiji cha Taratara walikamatwa na silaha aina ya short gun lemingi ston yenye namba NN 505220 V na risasi 30.

Aidha Masaki ameongeza kuwa watuhumiwa wote wapo mahabusu  na upelelezi unaendelea juu ya matukio hayo.

Post a Comment

 
Top