Menu
 


Polisi wakiwatawanya na kuwakamata baadhi ya waandamanaji hao katika manispaa ya Songea baada ya wakazi wa manispaa hiyo wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki kuandamana hadi ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma kupinga mauaji ya watu yanayoendelea kwa kasi mjini humo ambao hadi sasa jeshi la polisi halijafanikiwa kuwakamata wauaji.
MADEREVA PIKIPIKI WAKIWA WAMEFUNGA BARABARA YA SONGEA KWEWNDA TUNDURU KARIBU NA MLANGO WA KUINGILIA OFISI YA MKUU WA MKOA WA Ruvuma,wakilitaka jeshi la polisi mkoa huo kuchukua hatua dhidi ya mauaji ya watu yanayoendelea mjini songea ambapo hadi sasa zaidi ya watu 8 wameuawa na watu wasiojulikana wengi wao wakiwa ni madereva wa pikipiki.
Mtu mmoja ambae Jina lake halija fahamika mapema akiwa amepigwa Risasi na Polisi na Kufariki Papo hapo mapema jana.
*******
Habari na mwandishi wetu.
Watu watatu wameuawa kufuatia vurugu kati ya polisi na raia mkoani Ruvuma ambapo kati yao wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na Jeshi la polisi na mmoja ameuawa kwa ajali ya pikipiki na wengine 41 wamejeruhiwa.

Katika vurugu hizo wananchi walikuwa wakitoa lawama kwa Jeshi hilo kushindwa kukabiliana na mauaji ya watu ambapo miili yao ilikuwa ikikutwa imenyofolewa baadhi ya viungo vya mwili.

Kutokana na hali hiyo leo hii Jeshi la polisi mkoani humo limewashikilia askari wake wanne kwa mahojiano zaidi kutokana na kusababisha vifo vya watu wawili kupitia vurugu hizo.

Awali kabla ya vurugu baadhi ya madereva wa pikipiki na wananchi wa mtaa wa Lizaboni walianza kujikusanya na kuanza maandamano kuelekea kituo kikuu cha polisi kilichopo karibu na uwanja wa majimaji mjini songea huku wakiimba nyimbo za kulilaumu jeshi la polisi kushindwa kudhibiti mauaji ya zaidi ya watu kumi na tatu huku mmiili yao ikinyofolewa baadhi ya viungo.

Baada ya vurugu hizo Mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Ole Sabaya amesema Serikali inalishughulikia suala hilo na kwamba wananchi wanatakiwa kushirikiana kwa karibu na Jeshi la polisi katika kudhibiti matukio hayo kutokana na vitendo hivyo kufanywa kwa usiri mkubwa, pia watendeji wa matukio hayo ni miongoni mwa wanajamii wenyewe.

Post a Comment

 
Top