Menu
 

 Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wamefariki dunia  Mkoani Mbeya, wakiwemo wawili waliokuwa wamepakizana watu watatu katika pikipiki moja maarufu kama mishikaki na kuanguka barabara ya Mbeya/Iringa, FebruarI  21 majira ya saa Tatu usiku.

 Ajali hiyo imetokea  maeneo ya Mabadaga wilaya ya Mbarali ambapo dereva  aitwae  Kilubai  Kisota (44) mkazi wa Matebete akiendesha pikipiki yenye namba za usajiri T 971 BVU ilisababisha kifo chake na abiria aitwae Amina (25) mkazi wa Ilemi jijini MBEYA

Pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi kwa abiria mwingine aitwae  Michael Kisota (26) ambaye amelazwa katika hospitali ya Chimala Missioni  na hali yake inaendelea vizuri pia miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo.

 Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi ambapo dereva alishindwa kuimudu pikipiki hiyo.

Aidha majira ya saa 2;30 usiku Februari  21 eneo la Mlowo wilaya ya Mbozi  mtu mmoja aitwae Hakimu Pendo (32) mkazi wa eneo hilo alipigwa na kunyang’anywa pikipiki yake na watu wasiofahamika

Mbinu iliyotumika na watu hao kukodi pikipiki  kwenda Mlowo ndipo walipofika eneo hili walimpiga na kunyang’anya pikipiki hiyo

Pendo amelazwa  katika hospitali ya Mbozi Mission ambapo Jeshi la Polisi  wanafanya msako mkali ili kubaini waliohusika ingawa namba na aina ya pikipiki haijulikani kwa mjibu wa Kamanda wa Jeshi hilo Advocate Nyombi .

Post a Comment

 
Top