Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Zaire Mwangonda  mkazi wa kijiji cha Ipinda na Kasto Mwaigega  mkazi wa kijiji cha Mbugani wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya  kupigwa na wananchi wenye hasira kali wakituhumiwa na wizi wa mabomba ya josho la kuogeshea ng’ombe ambayo ni mali ya wanakijiji.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakati wakiwa kwenye harakati za kukimbia na mabomba hayo ambayo walikuwa wameyafunga kwenye pikipiki ainaya T beater yenye namba za usajili T.981 BDP.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio na kuongeza kuwa licha ya watuhumiwa hao kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kutumia mawe kisha kuchomwa moto watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa bado hai na wamepelekwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema thamani ya mabomba ambayo yalitakwa kuibwa ni shilingi milioni nne laki tatu  na elfu ishirini.

Hata hivyo uchunguzi bado wa tukio hilo unaendelea.

Post a Comment

 
Top