Menu
 

Mlezi wa kituo cha Nuru Orphans Bi Amanda Fyabango akionesha malazi wanaolazwa watoto wanaookotwa mitaa na kuwalea kama familia moja, na kwamba kituo hicho kimeanza mwaka 2008 kikiwa na watoto wawili ambapo kwa sasa kinanjumla ya watoto 14. Aidha ameeleza chanzo kikuu cha watoto kutupwa ni kutokana na wananume kukataa mimba, kutelekeza wake zao na ugumu wa maisha. Ameongeza kuwa wanawake na mabinti wanapopata mimba wasiitoe.
 *******
Habari na Mwandishi wetu.
Wazazi na walezi wametakiwa kutowafungia ndani watoto wenye ulemavu na badala yake wametakiwa kuwapeleka shule ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma muhimu ili waweze kujitegemeaa hapo baadae.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inashughulikia vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa wanawake na watoto kata ya Sinde jijini hapa Bwana Imanuel Simoni wakati wa mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake kuhusu mchango wa asasi hiyo kwa jamii.

Amesema watoto wenye ulemavu wamekuwa wakinyimwa haki zao za msingi hali inayowapelekea kudumaa kifikra, kiafya na kielimu na hatimae kuishia kuwa ombaomba.

Post a Comment

 
Top