Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Maliatabu Bashiri mwenye umri wa miaka 65 mkazi wa kijiji cha Majengo wilayani Chunya mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na fimbo mwilini mwake baada ya marehemu kugonga nyumba ya mtuhumiwa wakati akiwa amelewa pombe.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema tukio hilo limetokea January 28 majira ya saa mbili za usiku ambapo marehemu alikosea njia na kwenda kuigonga nyumba ya Nsajigwa Mwakyando hali iliyompelekea Mwakyando kutoka nje na kuanza kumshabulia marehemu kwa viboko.

Kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa mtuhumiwa huyo Marehemu Maliatabu Bashiri alipata majeraha mbalimbali kwenye sehemu za mwili wake na alifariki dunia jana wakati akiendelea kupata matibabu nyumbani kwake.

Hata hivyo mtuhumiwa alitoroka kijijini humo mara baada ya kusikia kuwa hali ya kiafya ya Maliatabu Bashiri imekuwa mbaya na kwamba Jeshi la polisi linaendelea kumtafuta Nsajigwa Mwakyando kwa tuhuma za mauji.

Post a Comment

 
Top