Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Whyson James Swilla (70), ameuawa kwa kutenganishwa kichwa na kiwili wili chake mita chache kutoka nyumbani kwake februari 5 mwaka huu.

Hata hivyo awali marehemu alifuatwa nyumbani kwake katika mtaa wa Londoni, Vwawa wilaya ya Mbozi na watu wasiofahamika lakini bila mafanikio walimkosa, na kumkuta mwanawe mwenye umri wa miaka 14 na kisha watu hao waliamua kuvunja mlango na  kuiba kuku.

Kwa upande wake mkazi mmoja Bi Nesi Mwambalo aliukuta mwili wa marehemu barabarani ukiwa umetapakaa damu na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Jaston Wega ambaye alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Vwawa na kuuchukua mwili wa marehemu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa uchunguzi na kisha mwili kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu.

Mazishi yamefanyika majira ya saa 8 mchana na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na mauaji hayo na chanzo chake hakijaweza kufahamika mara moja na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.

Post a Comment

 
Top