Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Sister Mapunda (40), mkazi wa kijiji cha Lungwa, Kata ya Isansa wilaya ya Mbozi mkoa ni Mbeya amefariki dunia baada ya kunywa sumu  Machi 10, Mwaka huu.

Mwanamke aliondoka nyumbani kwake kuelekea shambani majira ya saa 2 kamili asubuhi kwa ajili ya kung’oa maharage, na kurejea nyumbani hapo majira ya saa 3 asubuhi kisha kuingia chumbani kwake na kunywa sumu.

Baada ya kunywa sumu hiyo alimweleza mwanae kuwa kanywa sumu, hivyo mtoto huyo alienda nyumbani kwa bibi yake umbali wa mita mia tatu, na bibi huyo(mama wa marehemu) alipofika nyumbani hapo alimkuta binti yake hazungumzi kitu chochote.

Naye, bibi huyo alitoa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Viran Mbinile ambapo walichukua gari na kumkimbiza marehemu katika Hospitali ya Mbozi Mission, kwa ajili ya matibabu hata hivyo alifariki dunia katika Kitongoji cha Zelezeta mita chache kabla ya kufika Hospitalini.

Mwili wa marehemu ulipelekwa Kituo cha Polisi Mlowo, ambapo baada ya taarifa ya Polisi mwili ulikabidhiwa kwa ndugu zake na chanzo cha kifo chake hakijaweza kufahamika kwani marehemu ahakuweza kuacha ujumbe wowote.

Hata hivyo marehemu Sister alifiwa na Muwewe mwaka 2008 kijijini hapo.

Post a Comment

 
Top