Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mkazi mmoja wa Mbalizi, Wilaya ya Mbeya Vijijini Bwana Musa Mwambapa (25), amelazimishwa kula kinyesi cha binadamu baada ya kukamatwa ameiba kuku katika Kijiji cha Sisitila, Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea jana Machi 30 mwaka huu, majira ya saa nne asubuhi katika kijiji hicho pale mtuhumiwa alipoiba kuku mali ya Bwana Vedastus Jerome (45).

Baada ya mtuhumiwa kukamatwa wananchi wenye hasira kali walimtaka achague adhabu moja kati ya mbili, ambazo ni kumwagiwa mafuta ya petroli kisha kuchomwa moto au kula kinyesi cha binadamu ambapo bila kinyaa alichagua kula kinyesi cha binadamu kisha akaachiwa.

Hata hivyo juhudi kuwatafuta viongozi wa Kijiji hicho akiwemo balozi na Mwenyekiti wa kijiji hicho kugonga mwamba kwa vile walikuwa wamekwenda msibani eneo la Mbalizi na hazikuweza kupatikana hewa.

Post a Comment

 
Top