Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya Vijijini.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ford Mwakambonja (41) mkulima na mkazi wa Nyalwela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoani Mbeya ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za kuiba pikipiki.

Tukio hilo lemetokea majira ya saa tisa alasiri katika Kijiji cha Kimondo wilayani humo, ambapo kundi la wananchi walimkamata marehemu akiwa na pikipiki aliyoiiba mali ya Bwana Pius Jonas, kisha kumpika na kumuua papo hapo.

Wananchi hao hawakuishia hapo baada ya kumuua Ford na mwili wake kuuteketeza kwa kuuchoma moto na pikipiki aliyoiiba ikihifadhiwa katika Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Kimondo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Hata hivyo wimbi la wizi wa pikipiki limekithiri Mkoani Mbeya, ambapo baadhi ya madereva wameporwa na kuuawa hali inayowatia hasira wananchi pindi wanapowakamata wahalifu wa wizi huo.

Post a Comment

 
Top