Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo eneo la Iwambi Stella Farm, majira ya saa mbili usiku jana baada ya kugongana uso kwa uso magari mawili aina ya Hiace iliyokuwa ikitokea Mbalizi na Pick up iliyokuwa ikitokea Mbeya mjini kuelekea Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini. 

Hata hivyo mashuhuda waliofika eneo la tukio akiwemo mwandishi wa habari hii walifanya kazi ya ziada kuunasua mwili wa dereva wa gari aina ya Pick Up, baada ya magari hayo kukaa kutenganishwa kwa njia ya kawaida.

Chakushangaza zaidi uungwana haukuweza kufanyika kutoka na baadhi ya watu kukosa ubinadamu baada ya kusaidia kuunasua mwili huo, walikuwa waking'ang'aniana bidhaa mbalimbali zilizokuwemo kwenye Pick up.

Chanzo cha ajali hii kimetokana na ukungu na mvua kubwa ambayo imepelekea barabara kuwa na utelezi hali iliyosababisha Pick up kuhama njia na kugongana uso kwa uso na Hiace.

hata hivyo kikosi cha Usalama barabarani cha mkoani hapa kiliweza kufika eneo la tukio na kusaidi uokoaji.

*****KWA HABARI KAMILI ENDELEA KUFUATILIA MTANDO HUU*****.

Post a Comment

 
Top