Menu
 


Habari na Angelica Sullusi
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezindua kampeni za kuwania nafasi ya udiwani Kata ya Kiwira Wilayani Rungwe ambapo uchaguzi huo unakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo John Mwankenja aliyeuwawa kwa kupigwa risasi mwaka jana.
Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho Mbunge wa Viti Maalum Anna Mary Mallack amesema wananchi wa Kiwira wanahitaji mabadiliko ya kimaendeleo ambayo yanaweza kuletwa kupitia CHADEMA.
Naye Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigija amesema anaimani kubwa ya CHADEMA kupata ushindi katika kata hiyo kutokana na wananchi kuchoshwa na vitendo vinavyofanywa na Chama cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata hiyo, Lawlent Mwakalebule amesema kuwa ameamua kujitosa kuwania kiti hicho akiwa na umri mdogo ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwasilisha matatizo yao.

Post a Comment

 
Top