Menu
 

Kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimoro akiwa na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchi ya Zambia Bwana James Singoi  na viongozi wengine wa wilaya hizo katika mkutano wa ujirani mwema uliofanyika katika wilaya ya Mbozi hivi karibuni. Dhumuni la mkutano huo ilikuwa ni kuimarisha ulinzi na usalama mpakani pia kudhibiti uhamiaji haramu. (Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimoro na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bwana Levison Chilewa jana wamepata wakati mgumu kuwa jibu wananchi wa Kijiji cha Mlowo maswali yao, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

Baadhi ya maswali yaliyooulizwa ni gharama za nauli ya abilia katika mabasi kati ya Mlowo na Vwawa kutonzwa shilingi 1000/= badala ya shilingi 500, kushindwa kupatikana kwa mbolea, kudaiwa mara mbili ushuru wa mazao na viwanda, ushafu uliokithiri katika Soko la Mlowo, pamoja na kushindwa kupewa hadhi ya mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo kutokana na ombi lao kuliwasilisha toka mwaka 2005.

Alipotakiwa kujibu maswali hayo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwana Chilewa alishindwa kutoa majibu ya kuwaridhisha wananchi hao hali iliyopelekea kuzomewa na kutishia mkutano kuvurugika, mpaka alipookolewa na Afisa Tawala wa wilaya hiyo Bwana Mpandachombo ambaye alimketisha chini na kumpa nafasi Mkuu wa wilaya kuyajibu maswali hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Kimoro alisema anakubaliana na wananchi hao hivi sasa, Mlowo kuwa ni Mamlaka ya mji kutokana na eneo hilo kukidhi sifa za kuwa mji kama vile barabara, hospitali, soko na ididi kubwa ya wakazi. Hivyo atahakikisha agenda hiyo anaifikisha mahala husika.

Hata hivyo wananchi wamesema kuwa hawanufaiki na  ushuru wa viwanda, kutokana na kutopewa marejesho yoyote yanayohusu mapato hayo kutokana na uwepo wa viwanda hivyo,

Mkuu wa wilaya Bwana Kimoro ameongeza kuwa ataangalia uwezekano ili wananchi hao kulipia ushuru wa eneo moja kama shambani au katika mji huo ili pia ili kusaidia uendelezaji wa mji huo.

Hikuishia hapo Mkuu huyo wa wilaya aliwaagiza Askari wa usalama wa barabarani wasimamie suala la nauli, kwani nauli halali ya kutoka Mlowo mpaka Mbozi ni shilingi 500/= badala ya 1000/= na kwamba atakayetoza zaidi nauli achukue namba na tiketi na kumfikishia ofisini kwake.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mlowo Bwana Yotamu Katule alimtaka Mkuu wa wilaya kuwaonya watendaji wake, kufuata maadili ya kazi zao na utawala bora ili kuleta amani katika mji huo, badala ya kukaa maofisini, na pia aliungana na wananchi kutoendelea kulipa ushuru baada ya wakala anayekusanya ushuru huo kutokuwa na imani naye na kijiji kutonufaika.

Wananchi hao waliendelea kulalamikia ujenzi wa choo cha soko cha matundu mawili kilichogharimu shilingi milioni 200, hali iliyowashangaza na kuashiria kuwepo kwa ubadhilifu mkubwa.

Mkuu wa wilaya Bwana Kimoro aliishia kwa kusema ataunda kamati ya kufanya uchunguzi kuanzia Machi 12, mwaka huu itakayofanya kazi kwa muda wa wiki moja na baada hapo ataitisha mkutano ili kutoa majibu yaliyosahihi kuhusiana na agenda zote zilizoainishwa kwake katika mkutano huo.

Post a Comment

 
Top