Menu
 


Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi.
******
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, amesema hayuko tayari kuona fedha za mfuko wa Jimbo zikipelekwa katika miradi isiyomalizika kutokana na kwamba miradi hiyo imekuwa ikianzishwa kwa lengo la kuwanufaisha watu wachahe.

Ameyasema hayo kupitia mikutano yake ya hadhara aliyoimaliza hivi karibuni jijini hapa ambapo amesema licha ya Serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwaletea wananchi wake maendeleo, fedha hizo zimekuwa zikiliwa na watu wachache.

Wakati huohuo amependekeza fedha hizo kutumika katika mradi mmoja ambao utaonekana badala ya fedha hizo kutawanywa katika miradi mingi isiyo tekelezeka.

Aidha Mbilinyi amesema kupitia fedha za jimbo tayari miradi kadhaa katika Kata 17 Jijini imetekelezwa ambapo ameitaja miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Sekondari ya Kata ya Iziwa, Jengo la utawala katika sekondari ya Pankumbi na Ofisi ya kisasa ya Kata ya Ghana ambayo imejengwa kwa thamani ya shilingi milioni 10.

Post a Comment

 
Top