Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mahakama kuu Kanda ya Mbeya imewahukumu kwenda jela miaka 8, watu wawili kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu na madawa aina ya PPF kinyume na sheria.

Mwendesha mashtaka wa serikali Christians Joans ndiye aliyesoma mashtaka mbele ya hakimu Monika Ndyekobora, amesema mchungaji Cosmass Mwasenga na Lusechelo Mwashilindi kwa pamoja walitenda kosa hilo Kijiji cha Mlowo wilaya ya Mbozi mnamo Februari 13 2009.

Akitoa mashtaka mwanasheria wa serikali amesema watuhumiwa hao walikuwa na mashitaka matatu ambayo ni kukutwa na viungo vya binadamu na hilo ni kosa kifukngu cha sheria 222 (A), pili wameshitakiwa kwa kosa la kula njama ya kuuza viungo hivyo ambalo ni kinyume cha 385 na kosa la tatu ni kukutwa na madawa aina ya PPF na sumu ya chupa 18 na chupa 14 za maji ya kuchanganyia ambalo ni kosa la sheria kifungu cha sheria  kifungu cha 37 (i) (A) na (B) kinyume na sheria ya madawa.

Hakimu Ndyekoba aliwatia hatiani washitakiwa hao kwa makosa yote matatu hivyo kuwaamuru kwenda Jela miaka 8 wote wawili ambao ni Mchungaji Cosmass Mwasenga na Lusechelo Mwashilindi pia hakimu alimuongeza miezi 6 Lusechelo au faini shilingi 2000/= kwa kosa la kutunza madawa hayo bila kibali endapo atashindwa kulipa faini.

Post a Comment

 
Top