Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mganga mmoja wa jadi aliyefahamnika kwa jina moja la Mgalah ameuawa na wananchi wenye hasira kali, katika mtaa wa Ilolo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Machi 11 mwaka huu majira ya saa.10 jioni.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Bwana Assah Lusoko amesema alikuta mabishano kati ya mganga huyo na mtu mmoja, ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja.

Hata hivyo wananchi hao baada ya kuona kijana huyo anaelemewa na Mganga, waliamua kumpiga hadi mauti yalipomfika na mwili wake kuhifadhiwa katika Hospitali ya serikali Vwawa wilayani humo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi kubaini waliohusika na tukio hilo.

Aidha, majira ya saa 9 kamili usiku eneo la Jacaranda jijini Mbeya mtu au watu wasiofahamika walivunja moja ya vyumba anavyoishi Afisa mauzo wa Kampuni ya Mwananchi Communication Bwana Bonventure Mwaunda (32), na kuiba pikipiki aina ya bajaji yenye nambari za usajili T 614 BSJ.

Kamanda Nyombi amesema Bwana Maunda aligundua kuibiwa kwa pikipiki hiyo baada ya kuvunja mlango na upelelezi wa tukio jili unaendelea ili kuwabaini watu waliohusika na tukio hili...

Wakati huo huo watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kukutwa na Kate 23 za bangi sawa na gram 615.

Watuhumiwa walikamatwa na Polisi waliokuwa doria eneo la Mwanjelwa, jijini Mbeya  Machi 11, mwaka huu majira ya saa kumi na mbili na dakika kumi na tano jioni.

Kamanda Nyombi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Anthon Francis (21), mkazi wa Sae, Staford Joel (23) mkazi wa Makunguru jijini hapa na watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamilika.

Post a Comment

 
Top