Menu
 


Habari na Angelica Sullusi, Mbeya
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zuberi Zitto Kabwe amesema sera mbovu za Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimechangia kuongezeka kwa umasikini uliokithiri kwa wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini.

Zitto amesema hayo jana wakati wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani kupitia CHADEMA, Laurent Mwakalebule katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kiwira uliofanyika katika mji wa Kiwira Rungwe.

Amesema kuwa licha ya Serikali kutangaza kukua kwa  uchumi wa nchi kila mwaka, idadi ya watu masikini inazidi ongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na taarifa ya Serikali ya maendeleo ya uchumi inaonyesha kuwa mwaka 2007 watanzania milioni 11 walikuwa masikini wa kutupwa na kuwa idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia milioni 14 kwa mwaka jana.

Amesema kuwa iwapo Watanzania hawataamka sasa kwa kukiondoa Chama Cha Mapinduzi(CCM) madarakani,basi idadi ya masikini itaongezeka mara dufu katika miaka michache ijayo kwa kuwa umasiki wa watanzania unasababishwa na sera mbovu za chama hicho.

Zitto amewataka wakazi wa Kata ya Kiwira kuanza kuleta mabadiliko hayo kwa kumchagua mgombea wa Chadema, ili akasimamie na kutetea maslahi ya wananchi kwenye halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.

Post a Comment

 
Top