Menu
 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), baada ya kumaliza mbio zake mkoani Rukwa.
******
 Habari na mwandishi maalum.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amekemea vitendo vya baadhi ya watumishi katika idara za serikali kugeuza ofisi zao vijiwe vya kupigia porojo badala ya kufanya kazi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa serikali ya wilaya ya Rungwe, watumishi wa halmashauri, viongozi wa dini pamoja na baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema wapo baadhi ya watumishi ambao wamekuwa wakiendeleza mazungumzo yasiyo na tija kwenye ofisi za Umma jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kuzorota kwa shughuli za kimaendeleo.

Aidha amewataka watumishi wa Serikali, watendaji na madiwani kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuboresha utendaji kazi wao badala ya kuwekeana matabaka ya kiutendaji.

Post a Comment

 
Top