Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja amefariki dunia mkoani Mbeya baada ya kupingwa na wananchi wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi wa nyanya shambani.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 2 kamili asubuhi katika eneo la Uyole jijini Mbeya baada ya marehemu Emmanuel anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 26 au 27, kutuhumiwa kuiba nyanya katika shamba la Jacob Wilson (41), ambaye ni mkuliwa na mkazi wa Uyole jijini Mbeya.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mmiliki wa shamba hilo Bwana Jacob kwa mahojiano zaidi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Jeshi hilo Advocate Nyombi,  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya.

Wakati huo huo mwili wa mwanafunzi anayedaiwa kuuawa kwa kipigo cha Askari wa Jeshi la Polisi kijiji cha Lupa Tingatinga umezikwa Februari 4 majira ya saa tatu usiku baada ya kufanyiwa uchunguzi  katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini hapa, baada ya wazazi kuususia mwili wa marehemu Saidi Msabaha. kwa muda wa siku mbili katika Kituo cha Polisi Lupa.

Kamanda Nyombi alitoa gari kusaidia shughuli ya mazishi baada ya kikao cha ulinzi na usalama wilaya ya Chunya chini ya Mkuu wa wilaya hiyo Deodatus Kinawiro na wananchi kuridhia askari waliohusika na mauaji kukamatwa.

Post a Comment

 
Top