Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Ikiwa ni siku 7 zimepita toka maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani Bi. Agnes Mkwila (51), mkazi wa kijiji cha Matebete Kata ya Itamboleo wilaya ya Mbarali amechomewa nyumba usiku wa kuamkia Machi 13, mwaka huu majira ya saa 3 usiku.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapangala Bwana Kijukali Ngekyee (48), ndiye anatuhumiwa kutenda kosa hilo kutokana na mtoto wake anayejulikana kwa jina la Papaa Kijukali (20) kumpa mimba mtoto wa Bi Agnes aitwaye Naselian Tetea (17) ambaye ni mwanafunzi.

Mtuhumiwa baada ya kuona suala hilo limeripotiwa Polisi alifanya njama za kumvizia kaka wa Naselian aitwaye Elisha Tetea (35) na kumjeruhi vibaya alipokuwa kwenye lindo Februari 5 mwaka huu, siku moja kabla ya mwanae Papaa kupelekwa mahakama ya wilaya hiyo iliyopo Rujewa kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi.

Mwenyekiti huyo ameendelea kutumia madaraka yake vibaya kwa kumtishia mama huyo kama ataendelea kuendesha kesi hiyo atahakikisha anamwaga damu ya mama huyo.

Hata hivyo taarifa za vitisho vya mwenyekiti Kajukali vimeripotiwa katika Kituo cha Polisi Chimala, ambapo Bwana Elisha Tetea alijibiwa kwamba endapo atafanya fujo ndipo polisi watamkamata.

Wakati huo huo walalamikaji wamefungua jalada katika Kituo hicho cha polisi namba CHI/RB/166/14/3/2012, ambapo wakati wowote watafikishwa mahakamani.

Post a Comment

 
Top