Menu
 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), baada ya kumaliza mbio zake mkoani Rukwa.
****** 
Habari na Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya maonyesho ya wakulima(nanenane)Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Abbas Kandoro amewataka viongozi wa Chama cha wakulima katika kanda hiyo(Taso) kuhamasisha wanachama kujiunga na chama hicho ili kujijengea uwezo wa kuandaa  maonyesho hayo bila kutegemea msaada wa Serikiali.

Kandoro ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya maonyesho ya nanenane ambayo hufanyika kila mwaka kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya na kushirikisha wakulima kutoka mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.

Amesema kuwa umefika wakati ambao chama hicho kinapaswa kusimama kwa miguu yake na halmashauri ambazo kwa sasa ndizo zinazochangia sehemu kubwa ya maandalizi ya maonyesho hayo  zikabaki kusaidia pale kinapokwama.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Beatha Swai ameishangaa Taso kwa madai kwamba hata wakati wa maonyesho wanachama wake hawaonekani na badala yake mabanda ya maonyesho hujaa washiriki wanaoletwa na Halmashauri.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Taso Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Zeno Nkoswe ameiomba Serikali kupitia halmashauri zake kuendelea kukisaidia chama hicho kuandaa maonesho hayo kwa madai kuwa bado hakijawa na uwezo wa kuendesha mambo yake chenyewe.

Post a Comment

 
Top