Menu
 

Habari na Bomba FM, Mbeya.
Umoja wa wafanyabiashara katika soko la mwanjelwa jijini mbeya wamelalamikia kutokamilika kwa soko hilo.

mwenyekiti wa umoja huo Charles Syonga amesema muda ulioongozezwa wa miezi sita umekamilika mwezi Februari mwaka huu lakini hakuna dalili za kukamilika kwa soko hilo.

aidha amesema kumekuwepo kwa taarifa za ugawaji wa siri wa vyumba vya biashara ndani ya soko hilo na kuzua kwa malamiko kutoka kwa wafanyabiashara wengine.

Naye katibu wa umoja huo Janson Mtupwa amesema kutokana na hali hiyo wafanyabiashara hao wanalazimika kulipa riba za mikopo bila ya kuwa na uzalishaji unaofaa.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya Dokta Samweli Lazaro amesema hakuna ugawaji wa vyumba vya biashara ndani ya soko hilo na kuongeza kuwa taarifa za ugawaji wa vyumba hivyo itatolewa kupitia matangazo.

Post a Comment

 
Top