Menu
 

Habari na Angelicia Sullusi, Mbeya.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Wilaya ya Chunya, George Mtasha ameweka wazi azma yake ya kumpeleka mahakani Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini John Mwambigija ‘Mzee wa upako’kutokana na tuhuma alizomwelekezea za kupokea rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mtasha amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kutopata majibu ya barua yake ya  februari,2 mwaka huu akiiandikia ofisi ya chadema Mkoa,Mwambigija na nakala makao makuu ya chama ikimtaka Mwambigija kufuta ama kuthibitisha kauli yake aliyoitoa Januari,11 mwaka huu katika kikao cha mashauriano cha Mkoa kilichoendeshwa chini ya Katibu Mkuu wa Chadema Taifa,Dk.Wilbroad Slaa.

Mtasha amesema kuwa katika kikao hicho Mwambigija aliwaambia wajumbe kuwa Mtasha alihusika na kupokea kiasi cha shilingi  milioni moja na nusu kutoka kwa Mbunge wa jimbo wa Songwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo, Philipo Mulugo kwa lengo la kukihujumu chama.

Amesema kuwa licha ya kumtuhumu kupokea fedha hizo Mwambigija alidai kuwa Mtasha alikihujumu chama hicho katika jimbo la Songwe baada ya kumkatalia kuchukua fomu aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chadema Twina.

Amesema kutokana na tuhuma hizo alimtaka Mwambigija kuomba radhi ama kukanusha tuhuma hizo ambazo anadai si za kweli ifikapo machi,15 mwa huu,lakini hadi sasa hajapata majibu kutoka sehemu yeyote licha ya kupeleka nakala hizo ngazi za juu za chama.

Aidha,Mtasha ameonya kuwa endapo chama kitafumbia macho watu kama hao wenye tabia za kuendekeza majungu na fitina zisizokuwa na tija kwa malengo yao binafsi huku wakiwapakazia wenzao maneno kwa lengo la kujipatia umaarufu chama kitapoteza mwelekeo.

Amesema yeye hayuko tayari kuona chama ambacho yeye ni moja wa waanzilishi viongozi hapa Mbeya,kikisambaratika kwa ajili ya mtu mmoja anayechafua wenzao,ili hali wananchi wanakikubali na kukiamini.

Bomba Fm imewasiliana kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Chadema Taifa,Dk.Wilboard Slaa aliyeko katika kampeni za uchaguzi mgodo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki ambapo alisema kuwa hajapokea barua yeyote toka kwa Mtasha.

Katika kesi hiyo Mtasha anamdai Mwambigija fidia ya shilingi milioni 80 pamoja na kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi hiyo.

Post a Comment

 
Top