Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Watu wawili wafanyakazi wa kampuni ya Maramba Brokers ya jijini Mbeya wamefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa tuhuma za kuuza mali za Omary Lubalile kinyume na agizo la Mahakama.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Zabibu Mpangule mwanasheria wa Serikali Achelesi Mlisa amesema mwezi Januari kumi na mbili washtakiwa Betha Mbilinyi na Adeni Kenani Mwamalekele waliuza vitu vya thamani ya shilingi laki saba na nusu vinavyomilikiwa na Omari mkazi wa Block Q mtaa wa mkombozi kinyume na kifungu cha sheria namba 326 kifungu kidogo cha kwanza sura ya 16 cha marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo washtakiwa wakilikana shtaka hilo na wamerudishwa rumande kwa kukosa wadhamani wenye mali zisizo hamishika zenye thamani ya shilingi milioni tano na barua kutoka kwa mtendaji wa kata wanako ishi.

Kesi hiyo itasomwa tena machi kumi na tatu mwaka huu.

Post a Comment

 
Top