Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Wafanyakazi wawili wa kituo cha mafuta cha GAPCO kilichopo kata ya Sisimba eneo la uhindini wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya kwa tuhuma za wizi wa fedha taslimu shilingi milioni kumi na nne laki saba na elfu saba mia mbili tisini na tano.

Akisoma shtaka hilo Mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Seif Kulita mwanasheria wa Serikali Lugano Mwakilasa amesema washitakiwa Aroni Msangi na Albato Chipeta wote wakazi wa Soweto waliiba fedha hizo wakiwa kazini ambapo kosa hilo ni kinyume na kifungu cha Sheria namba 265 na 271 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Washtakiwa wamekana shtaka hilo na wamerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini wawili ambapo kila mmoja awe na fedha shilingi milioni tatu na mmoja kati yao awe ni mtumishi wa Serikali.

Kesi hiyo itasikilizwa tena machi kumi na nne mwaka huu.

Post a Comment

 
Top