Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Watu wawili waliokuwa wafanyakazi wa Kampuni ya Ilasi, iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, wamefikishwa mahakamani kujibu shtaka la kumuibia mwajiri wao.

Mshtakiwa wa kwanza ni Issa Jackson Msukwa na wa pili ni Matisho Wilson, ambapo kwa pamoja wanatuhumiwa kuiba starter mbili za magari aina ya Scania mali ya Lingson Chaula zenye thamani ya shilingi 2,980,000, Desemba 9 mwaka 2011 majira ya saa sita mchana.

Watuhumiwa wanadaiwa kuzifungua starter hizo katika magari yenye nambari za usajili T 265 BEN na T 191 AVL, ambapo waliyaacha katika kituo cha mafuta kinachomilikiwa na Lingson Chaula na kisha kuondoka ambapo walikamatwa Mlowo wilayani humo, wakiwa hawana starter hizo.

Kwa upande wake mlalamikaji amesema watuhumiwa awali walikiri kwamba wameiba lakini anashangaa wanapokataa mahakamani, pia wao ndio walikuwa wahusika wakubwa wa matengenezo ya magari yote.

Shahidi wa kesi hiyo Dickson Mwamlima (35) amesema anawatuhumu watu hao kwa urasimu waliokuwa wakiufanya siku hiyo na kisha wakatokomea na kukamatwa eneo la Mlowo wilayani hapo.

Post a Comment

 
Top