Menu
 

Kituo cha Magari ya abiria aina ya daladala kilichopo eneo la Kabwe jijini Mbeya.
******
Habari na Mwandishi wetu.
Mwenyekiti wa chama cha madereva wa daladala zifanyazo safari zake Mwanjelwa Mbalizi bwana Julius Pius amewataka wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri kufanyia matengenezo magari yao ili kuepusha ajali zisizo za lazimika.

Ameyasema hayo katika kikao cha madereva wa daladala hizo kilichofanyika katika ukumbi wa kangaroo uliopo Iyunga jijini Mbeya.

Amesema katika kukabiliana na ajali zisizo za lazima wamiliki hawana budi kufanyia marekebisho magari yao ikiwa ni pamoja na madereva wa magari hayo kuheshimu na kutii sheria za barabarani.

Wakati huohuo ameiomba halmashauri ya jiji la Mbeya kujenga kituo kingene cha daladala eneo la Kadege kutokana na kituo kilichopo sasa kuelemewa na magari hali inayohatarisha kutokea kwa ajali.

Post a Comment

 
Top