Menu
 

Habari na Mwandishi wetu
Wakazi wa mtaa wa Isanga kati kata ya Isanga jijini Mbeya wamekuwa wakitozwa shilingi mia tano kila mmoja kwa  ajili ya kulipia pango la ofisi ya mwenyekiti wa mtaa huo.

Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wananchi wamesema wamekuwa wakichangia fedha hizo pasipo kupewa taarifa za mapato na matumizi ikiwa ni pamoja na kiwango kinachohitajika kwa ajili kulipia pango la ofisi hizo.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo Hasan Musa na Mzee Mbeye amesema kuwa fedha hizo wamekuwa wakichangishwa pasipo kupewa stakabadhi.

Bomba Fm iliwasiliana na afisa mtendaji kata ili aweze kutolea ufafanuzi suala hilo hata hivyo alisema kuwa jambo hilo lipo chini ya Diwani wa kata hiyo kupitia chama cha CHADEMA bwana Dor Muhamed Issa ambaye naye amesema kuwa Mkurugenzi wa jiji ndiye anayeweza kulitolea ufafanuzi suala hilo.

Post a Comment

 
Top