Menu
 


 Wanawake  Mbali mbali katika sherehe Hizo
Wanafunzi wakiwa Wanasikiliza kwa umakini Hotuba. (Picha na Mbeya yetu Blog)
******
Habari na Mwandishi wetu.
Wanawake wametakiwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiliamali ili waweze kujipatia kipato kitakachowawezesha kujikomboa kiuchumi.

Rai hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kikundi cha Tufikile Bi.Alesi Sanile wakati wa mahojino na Bomba Fm katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo yameadhimishwa kiwilaya katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Ilomba.

Amesema kupitia shughuli za ujasilia mali mwanamke anafurasa kubwa ya kupata kipato kwa kutengeneza mikoba, vitambaa, maua pamoja na unga wa lishe.

Aidha kuhusu mtaji Bi.Sanile amewataka wanawake hao kujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji na kwamba masherti ya mikopo kwa wanawake ni nafuu.

Post a Comment

 
Top