Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wawili wanaodaiwa kufanya mapenzi katika moja ya nyumba za wageni mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya wameshindwa kujinasua baada ya tendo hilo juzi.

Hali iliyosababisha kupelekwa katika Zahanati ya mji huo ambapo pia walishindwa kuachanishwa na kupelekwa katika Hospitali ya Serikali ya wilaya ya Mbozi.

Kufuatia taarifa hizo watu wengi walimiminika katika Hospitali hiyo na mtandao huu ulifanikiwa kuonana na Daktari Mkoma, ambaye ni msemaje wa hospitali hiyo, na kukanusha kuwa hakuna jambo lililojitokeza, hakuna watu wa aina hiyo waleopelekwa hapo.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mji huo wameendelea kusisitiza kuwa ni kweli kuna tukio la aina hiyo na kudai kuwa kwa sasa watu hao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya.

Mtandao huu unaendelea kufuatilia zaidi ili kuweza kubaini undani na ukweli wa sakata hili, ikiwa ni uvumi wa pili kutokea mkoani hapa, ambapo tukio la  awali lilitokea wilayani Kyela lakini ukweli ulithibitisha kuwa ni uvumi baada ya kudaiwa kuwa walipelekwa katika hospitali hiyo ya Rufaa.

Wawili hao wanadaiwa kuwa ni mume wa mtu na mke wa mtu..

Post a Comment

 
Top