Menu
 

 Basi la Prince Muro namba za usajiri T 485 BQV, liliacha njia na kupinduka hali iliyopelekea kusababisha kifo cha Dausdedit Joseph (29) na abiria 14 waliokuwa wakisafiri kupitia basi hilo kutoka Dar es salaam kuelekea Tunduma kujeruhiwa Machi 19 mwaka huu majira ya saa 2:30 katika Kijiji cha Senjele Wilaya ya Mbozi .
Hivi ndivyo mwonekeno wa damu za abiria na taswira ya viti vilivyoharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyotokea Machi 19 mwaka huu majira ya saa 2:30 katika Kijiji cha Senjele Wilaya ya Mbozi
Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipotaka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili
Muonekano wa gari hili la mizigo lenye nambari za usajiri T 664 ABB lililokuwa na tela namba T 402 AGW ambalo limeharibikia bara barani.
Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu. (Picha kwa ushirikiano wa Ezekiel Kamanga na Joseph Mwaisango).
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu wanne wamefariki dunia Mkoani Mbeya kwa matukio wanne tofauti tofauti, likiwemo la mwanamke kufumaniwa na kupingwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.
 Tukio la hilo limetokea katika Kijiji cha Ndaga Wilaya ya Rungwe majira ya saa nne asubuhi ambapo Sharuna Dimon (30), ambaye ni mke wa mtu aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani, baada ya kukutwa akifanya mapenzi Yohana Mwazanga (35) ambaye ni dereva na mkazi wa kijiji hicho.

Hata hivyo Bwana Yohana amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na amelazwa katika Hospitali ya Igongwe wilayani humo na watu wawili Geophrey Hezron (21) na Bahati Mussa (35) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi .

Kamanda Nyombi amesema chanzo cha mauaji hayo kinatokana na wivu wa kimapenzi.

Ameongeza kuwa tukio la pili limetokea Machi 17 mwaka huu, katika Kijiji cha Isecho Kata ya Kwimba Wilaya ya Chunya, ambapo Flavian Otto (50) ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamisha na kisha mkono wa kushoto kutokomea nao kusikojulikana.

Amesema watu hao walimvamia marehemu nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku na chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni imani za kishirikina, kwani kwa mara kadhaa marehemu alikuwa akituhumiwa kujihusisha na imani hizo.

Kamanda Nyombi amesema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwambani wakati upelelezi nao ukiendelea

Tukio la tatu limetokea Kitongoji cha Igumila, Kijiji cha Ishata Wilaya ya Ileje, mwananchi mmoja Jumapili Kasege (32), aliuawa kwa kukatwakatwa kichwani na kitu chenye ncha kali.

Kwa mujibu wa Kamanda Nyombi amesema marehemu alikuwa akitumikia kifungo cha nje cha miaka miwili kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili marehemu baada ya kutishia kuua kwa kutumia na chanzo cha kuawa kwake hakijaweza kufahamika mara moja, na upelelezi wa tukio hili unaendelea.

Aidha Machi 19 mwaka huu majira ya saa 2:30 katika Kijiji cha Senjele Wilaya ya Mbozi basi linalomilikiwa na Prince Muro lenye nambari za usajili T 485 BQV, liliacha njia na kupinduka hali iliyopelekea kusababisha kifo cha Dausdedit Joseph (29) na abiria 14 waliokuwa wakisafiri kupitia basi hilo kutoka Dar es salaam kuelekea Tunduma kujeruhiwa.

Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa basi hilo na Lori lenye nambari za usajiri T 664 ABB lililokuwa na tela namba T 402 AGW lililokuwa limeegeshwa baada ya kuharibika na dereva wa basi na wakati akilikwepa lori na mbele kulikuwepo na lori jingine na alipojaribu kusimama basi liliacha njia na kupinduka.

Post a Comment

 
Top