Menu
 


*Mmoja aishi naye kama mkewe.
*Mkuu wa shule aogopa kutoa taarifa, akihofia usalama.
*Wazazi watafutwa ili wamalizane.

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bara, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Martin Ntwinzi amewapachika mimba na kuwazalisha wanafunzi wawili wa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo, ambao wote wawili wamejifungua hivi karibuni hali iliyowapelekea kukatisha masomo na mmoja kuishi naye kama mkewe.

Mwanafunzi wa kwanza anayefahamika kwa jina la Anifa Zyemba(16), wazazi wake Bwana Watson Zyemba na mdogo wake Samora Zyemba hawajui la kufanya kutokana na Afisa mtendaji huyo kushirikiana na viongozi wenzake wa serikali ya  Kijiji na Kata kuwatishia amani wananchi waliobaini vitendo hivyo.

Mmoja wa wananchi hao ambaye pia alibomolewa nyumba yake kisha kuteketeza kwa moto kila kitu kilichokuwemo katika nyumba hiyo, vikiwemo vifaa vya wanafunzi wawili wa Bwana Jumapili Mwampamba ambao hivi sasa wamesitisha kwenda shule kutokana na karo zao kuteketezwa.

Anifa amejifungua mtoto wa kiume miezi miwili iliyopita na kupewa jina la Christopher Martin Ntwinzi, na kiongozi huyo amekuwa akiishi na mwanafunzi huyo kama mkewe.

Aidha uchunguzi umebaini Afisa mtendaji huyo Bwana Martin pia amemkatiza masomo mwanafunzi mwingine wa Kidato cha pili katika shule hiyo aitwaye Jane Myala(19), ambaye mtoto wake alijifungulia njia Machi 31 mwaka huu majira ya saa tatu usiku akiwa na mama yake anayefahamika kwa jina la Asha Mwashamba, wakati wakielekea Kituo cha Afya cha Itaka kwa miguu kutokana na ukosefu wa pesa ya usafiri.

Hata hivyo mtoto huyo alifariki Aprili 8 mwaka huu na mazishi kufanyika siku hiyo ambapo na Afisa mtendaji huyo huyo hakuhudhuria mazishi.

Baba mzazi wa mwanafunzi huyo Bwana Menson Kalwelo Myala, mkazi wa Maninga, Kata ya Bara amesema ameshindwa la kufanya kutokana na kuuza mifugo na mazao yake, ili kumsomesha mwanae lakini kiongozi huyo amemharibia maisha mtoto wake na kumpa vitisho endapo atafichua uovu wa mtendaji huyo.

Mbali na hilo Afisa mtendaji huyo amewatelekeza wake zake wawili katika mtaa wa Isangu uliopo Vwawa, huku akifanya uharibifu mkubwa wa maisha ya wanafunzi kijijini hapo na wakati mwingine kutumia vibaya Ofisi ya kijiji katika vitendo vya ngono au nyumbani kwa Bwana Godwin Kabulu alikopanga.

Ntwinzi amekuwa akifanya mapenzi na wanafunzi hao bila woga kutokana na dhamana aliyopewa na Serikali wala hofu ya maradhi ya ugonjwa wa UKIMWI, ambao mpaka sasa hakuna chanjo wala tiba.

Katika hali ya kusikitisha Mtendaji huyo amejaribu kuitoa mimba ya mwanafunzi Jane Myala ilipokuwa na miezi mitano lakini haikuwezekana, na kabla ya kiongozi huyo kuhamia kijiji cha Bara alikuwa katika kijiji cha Hangomba ambako alihamishwa kutokana na kuhamasisha vurugu na mauaji ambapo tabia hiyo hivi sasa ameanza kuzileta kijijini hapo.

Wakati huohuo Afisa mtendaji huyo amekuwa akilindwa na baadhi ya viongozi wenzake kata na kijiji akiwemo diwani wa kata hiyo kwa mwavuli wa wizi wa mifugo huku wakificha maovu ya kudhoofisha maendeleo katika kata hiko sambamba na wilaya hiyo.

Post a Comment

 
Top