Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Mtu mmoja amefariki dunia Mkoani Mbeya baada ya kutokea kwa ajali barabarani, katika, Kijiji  cha Ndaga, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Aprili 10 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi.

Tukio hilo limetokea barabara ya Mbeya/Tunduma ambapo lori lenye nambari za usajili T 898 AHW aina ya Isuzu lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Deus Singinali  (28), mkazi wa Kikondo, Wilaya ya Mbeya Vijijini, lililomgonga mtoto aitwaye Winny Raston (5) wanafunzi wa Chekechea shule ya Msingi Ndaga na kumsababishia kifo papo hapo.

Aidha dereva wa gari hiyo amekamatwa na gari hilo katika Kituo cha Polisi Kiwira, na mwli wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Igogwe, wilayani humo na chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Alitelius Lusungu (23) mkazi wa Vwawa, Wilaya ya Mbozi baada ya kukutwa na kete 43 za bangi sawa na gramu 215 eneo la Mlowo wilayani humo majira ya saa 11:30 jioni Aptili 11 mwaka huu.

Hata hivyo mtuhumiwa ni muuzaji na mvutaji wa bangi, ambapo alikuwa na kete hizo kwenye maungo baada ya kupekuliwa .

Matukio yote yamethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Barikiel Masaki, ambapo amesema uchunguzi wa matukio yote mawili hayo unaendelea.

Post a Comment

 
Top