Menu
 

 Familia ya Bibi Harusi Ikupa Mwalukosya (29) katika picha ya pamoja nje ya nyumba yao siku moja baada ya harusi kutofungwa kutokana Ukata, uliopelekea Bwana harusi Mwalimu Gervas Shihamba Makambuya (29), kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya nauli ya kumfirisha Bibi harusi pamoja na wapambe.
 Bibi harusi Ikupa Mwalukosya (kushoto) akiwa na Mchungaji Nelusigwe Ikuka Mwangosi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Jimbo la Mwakaleli, akimfariji bibi harusi baada ya bwana harusi kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya usafiri.
 Bwana harusi Mwalimu Gervas Shihamba Makambuya.
Ukumbi wa Kiwira Motel ukiwa wazi, baada ya kupambwa na licha ya maharusi kutotokea lakini sherehe iliendelea bila maharusi kuwepo.

Hitimisho:-Bwana harusi chanzo cha harusi kutofungwa kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri na washenga wake ambao ni Bwana Amoni Mwangosi ambaye ni mshenga wa Bibi harusi na Bwana Angolile Mwakisilwa ambaye ni mshenga kwa upande wake wa Bwana harusi.

Kwa uapnde wake wa Mzazi wa Bibi harusi Mzee Akimu Mwalukosya, amesema hana kinyongo bali yaliyopita si ndwele na wagange yajayo kwani makosa yaliyofanyika yanazungumzika.

Hata hivyo kamati ya sherehe ya bwana harusi itakutana kesho(jumatano) kupata hatima ya harusi hiyo.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mwakaleli)


Post a Comment

 
Top