Menu
 

 Katibu tawala mkoa wa Mbeya akisoma hotuba ya mkuu wa mkoa huo Abbas Kandoro alipomwakilisha kufungua kutano wa 12 wa chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku wilayani Chunya(CHUTCU)
 

WAKULIMA wa zao la tumbaku wamehimizwa kuanza kujikita katika kilimo cha mazao mbadala kutokana na zao hilo kuendelea kupigwa vita na wanaharakati mbalimbali duniani.

Katibu tawala mkoa wa Mbeya Marium Mtunguja amesisitiza hayo kwenye mkutano wa 12 wa chama kikuu cha ushirika wa wakulima wa tumbaku wilayani Chunya(CHUTCU).

Mtunguja alisema kauli hiyo hailengi kukataza kilimo cha zao hilo bali kuanza kuchukua tahadhari kwakuwa hakuna ajuaye nini yatakuwa matokeo ya hoja zinazojadiliwa na kupiganiwa na wanaharakati wanaopinga uvutaji wa sigara.

Aliyataja mazao yanayoweza kupewa nafasi na kuleta manufaa makubwa kwa wakulima kuwa ni pamoja na ufuta unaostawi katika ardhi ya wilaya ya Chunya,ufuta na alizeti.

Alisisitiza pia CHUTCU kuona uwezekano wa kuanzia chama cha kuweka na kukopa (Saccos) ili kuwawezesha wanachama kuachana na mikopo iliyo na riba kubwa kutoaka katika taasisi kubwa za kifedha.

Katibu tawala huyo aliwataka wanaushirika kuhakikisha wanaviimarisha vyama vyao ili visishuke na kufa kama ilivyotokea kipindi cha miaka ya nyuma badala yake wajiwekee mikakati ya kuviendelea na kuwa na nguvu zaidi.

“Tuwe tunajiuliza ilikuwaje vyama vya ushirika vikafa.Sababu zipi.Ni kutokana na uongozi mbovu uliojikita katika kuchukua mikopo mikubwa na kuitumia vibaya kinyume na utaratibu sahihi. Sasa tusikubali kurudi huko.Sasa tusonge mbele”.

Alibainisha kuwa kuendelezwa kwa vyama hivyo kutakuwa chachu ya mafaniko kwa mtu mmoja mmoja na pia wilaya kwa kukuza uchumi utakaowezesha kufanikishwa kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo hasa elimu na makazi bora.


Kwa upande wake mwenyekiti wa CHUTCU Sebastian Mogela alikiri ushirika kuendelea kuyategemea makampuni ni kuchelewa kupiga hatua kimaendeleo akisema yapo kwaajili ya kufanya biashara yapate faida na si kutoa misaada kwa wakulima.

Mogela alisisitiza umuhimu wa chama kikuu hicho kuwa na maofisa uganiwake ili waweze kusimamia kwa karibu kilimo hicho na kuleta manufaa zaidi kwa wakulima badala ya Kuendelea kutumia wataalamu wa makampuni yanayonunua tumbaku.

“Haiwezekani tukajitegemea kwa pembejeo pekee wakati wataalamu wanaosimamia matumizi ya pembejeo hizo wanatoka kwingine. Lazima usimamizi wake utalenga kuinufaisha kampuni yake na wala siyo sisi”.

Post a Comment

 
Top