Menu
 

Ni kama ndoto! siku, wiki, mwezi  hadi leo hii ChingaOne inapotimiza mwaka mmoja tangu irushe habari yake ya kwanza tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita. 

Nitakuwa mchoyo wa shukrani kama sitatambua uwepo wa Wadau wangu wote walionifanya nisimame na kunipa nguvu siku zote 365! haikuwa kazi rahisi kwangu bila wao kunishika mkono, bila wao kunipa moyo na kunikumbusha kila nilipoonekana kuchoka na kuhisi kushindwa! "Uwepo wangu ni kwa ajili yenu

Nachukua fursa hii pia kuwashukuru ndugu , jamaa na marafiki wote walionivulimilia sana kwa  kukosa uwepo wangu kila waliponihitaji  kwa sababu ya kuiimarisha kurasa yangu! "Nawapenda sana kuliko mnavyofikiria"

Sitaweza kuwasahau Mablogger wenzangu wote kwa kunifanya nifike hapa nilipo kwani changamoto zenu kwangu zimekuwa kama moto  na kichocheo cha mimi kubaki imara na kufanya ChingaOne izidi kusimama!  "Mapambano bado yanaendelea."  Happy Birthday www.chingaone.blogspot.com

Post a Comment

 
Top