Menu
 

Na Kenneth Ngelesi, Mbarali
Ucheleweshaji  wa fedha za ruzuku kutoka Serikali  kuu  inaelezwa kuwa ndiyo kikwazo kikubwa cha utekezaji wa miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika wilaya Mbarali Mkoani Mbeya.

Hayo yalibanisha hivi karibuni na  Mwenyekiti wa Hamashauri ya wilaya ya Mbarali Kenneth Ndingo mjini Rujewa wakati wa kikao  cha baraza la madiwani na wakuu wa idara zote kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo mjini Rujewa na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya Kanali msaafu Cosmas Kayombo

Katika kikao hicho mwenyekiti huyo alisema licha ya nadiwani kupisha bajeti ya mwaka 2011-2012 kwa ajili ya utekeleza wa miradi mbali mbali lakini imekwama kutekelezwa kutokana na fedha walizo omba kutoka serikari kuu kutofika kwa wakati.

Akizungumza mbele ya madiwani hao Ndingo alisema kuwa katika bajeti ya mwaka huo wa fedha hamashauri ilikusidia kujengamiradi mbalimbali ikiwa ni pamoja miundombinu ya barabara, umwagiliaji, majosho, maramba, shule za msingi na sekondari na ujenzi wa vituo vya afya  pamoja na jingo la utawala la idara ya afya lakini miradi hiyo haukute kelezwa kutokana na tatizo hilo,hata hivyo aliwaambia  madiwani hao kuwa miradi ipo katika hatua za kuanza kutekelezwa.

Aidha katika hatua nyingine madiwani hao waliomba kupewa ufafanuzi juu ya taasisi zinazo toa huduma a ukimwi katika kata hiyo zinatakiwa kuwajibika kwa nani kwani madiwani wamekuwa hawaelewa licha ya NGO hizo kuwa katika kata ambazo wao wanawa wakilisha wananchi.

Madiwani hao walizi lalamikiwa tasisi hizo zimekuwa hazitoi taarifa kwa madiwani ho kwa madi kuwa  zinawajibika kwa wafadhili wanao toa misaada kwa ajili ya ukimwi wilayani humo, katika wilaya hiyo kuna NGO’s  12 zinazo jihusisha na huduma ya ukimwi.

Katika suala la ukimwi baraza la madiwani liliazimia kuwa kila diwani anatakiwa kuwe mwenyekiti wa kamati ya ukimwi katika ngazi ya kata ili kuwa na taarifa kamili juu ya watu  tasisi zinazo toa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi na pia kuja watoto wanao someshwa na Tasisi hizo.

‘Unajua mwnyekiti tuna  NGO’S zinazo toa huduma ya UKIMWI katika wilaya yetu yenye kata kumi lakin taasisi hazijawa tayari kushikiana na sisi ndiyo maana inatuwia vigumu kwa waheshimiwa madiwani kuwa na taarifa kamili kuusu wagonjwa wa ukimwi pia hata watoto wanao wanao hudumiwa na  tasisi hizo,

‘Kwa hiyo mheshiwa mwenyekiti kuna kila sababu ya kutunga sheria ya kuhakikiasha NGO’S hizi tuna shirikiana nazo ili kuwapa nafasi madiwani kuwa na taarifa kamili juu tatizo hili katika wilaya yetu’ alisikika  moja wa Madiwani hao

Aidha katika hatua nyingene madiwani hao walionyeshwa kusitishwa na taarifa ya ujauzito kwa wanafunzi 15 katika shule sekondari Mengele na watuhumiwa kutochukuliwa na hatua za kisheria dhidi yao.

Naye Mkuu wa wilaya alisema aliwasihi wakuu wa idara kutowachukia madiwani hasda pale wanapo utekelezaji wa miradi kwani lengo lao ni kuwa kutaka kuijenga wilaya yao.

Alisema kuwa katika hali ya kaweaida kunaweza kukuwa na msuguano baina ya madiwani na watendaji wa serikali lakini dhamira yao iwe ni moja ya kuijenga Mbarali na sio kwa maslai yao binafsi kwa hiyo kuna kila sababu ya kuwa wavumilivu hasa katika shuguli za maendeleo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya Cosmas Kayombo alisema kuwa kwa ujumla wilaya ya Mbarali haiweza kuwa na tatizo la njaa kwani karibu wilaya zote zinazoizunguka kuna chakula cha kutosha tatizo la kutokuwa na chakula ni kutokana kuuzwa kwa bei ndogo hivyo wafanyabiashra wamekuwa wakisita kupeleka chakula kutokana na tatizo la bei kutowalipa.
Katika wilaya ya Mbarali kumekuwepo na tatizo la chakula katika baadhi ya vijiji na  kukwamisha shuguli mbalimbali za maendeleo kutokana muda mwingi kutuimia kutafuta chakula bada ya shughuli za maendeleo.

Post a Comment

 
Top