Menu
 


Habari na Angelica Sullusi, Mbeya
Walimu wapya walioajiriwa februari mosi mwa huu katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, jana walikusanyika nje ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ili kushinikiza kulipwa madai ya fedha za mizigo na mshahara wa mwezi Februari ambao hawajalipwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa mashariti ya kutotajwa majina yao walimu hao ambao ni wa shule za misingi na sekondari wamesema kuwa wamekuwa wakipewa kauli tofauti kutoka kwa watu tofauti juu ya madai ya malipo yao.

Wamesema kuwa awali walionana na Mkurugenzi Idd Jumanne na kuwahakikishia malipo ya madai yao yote ifikapoa aprili 3,lakini cha kushangaza siku hiyo ilipofika walielezwa kuwa wamsubiri kwani alikwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwenye kikao na baadaye majira ya saa 12 jioni walikuja maofisa elimu  wa Jiji,sekondari na msingi ambao waliongozana na vyombo vya usalama na kuwaondoa ofisini hapo.

Mkurugenzi Idd amekiri kuwepo kwa madai ya walimu hao na kusema kuwa kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma walimu wapya hawasitahili kulipwa fedha za mizigo bali wanalipwa shosho ya siku saba pamoja na nauli ambazo tayari wamekwishalipwa.

Kuhusu kutolipwa mishahara Idd amesema kuwa walimu wapatao wanne kati ya 184 ndio waliolipwa mshahara wa mwezi februari kutokana na kuingizwa mapema kwenye mfumo wa malipo ambapo wengine hawakulipwa mshahara wa mwezi huo lakini mwezi machi wameonekana walimu 151 ambao wamepata mshahara.

Amesema walimu 29 tu ndio waliokosa mshahara wa mwezi machi kutokana na taarifa zao kuwa na mapungufu wakati zikipelekwa wizarani tayari kwa malipo na kusema kuwa tayari fedha imekwishaandaliwa na halmashauri ili walimu hao walipwe mapema leo,na mara watakapokuwa wameingia katika mfumo wa komputa watazirejesha.

Idd amewataka walimu hao kuwa wavumilivu kwa kuwa taratibu za ujazaji wa fomu za madai ya malimbikizo ya mshahara wao wa mwezi februari zinafanyiwa kazi ili zitumwe hivyo wategemee kuzipata pamoja na mshahara wa mwezi Aprili.

Post a Comment

 
Top