Menu
 


Kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbozi Bwana Gabriel Kimoro akiwa na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchi ya Zambia Bwana James Singoi  na viongozi wengine wa wilaya hizo katika mkutano wa ujirani mwema uliofanyika katika wilaya ya Mbozi hivi karibuni. Dhumuni la mkutano huo ilikuwa ni kuimarisha ulinzi na usalama mpakani pia kudhibiti uhamiaji haramu. (Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Baraza la Madiwani wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya limefanyika Aprili 5 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, kwa ajili ya kujadili mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012 na kupitisha bajeti ya 2012/2013.

Baraza hilo lilifunguliwa na Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Gabriel Kimoro, ambapo amesema kuwa madiwani waondoe tofauti zao za kisiasa kwa nia ya kuijenga wilaya hiyo na kuleta maendeleo.

Aidha mkutano huo ulipitisha bajeti ya shilingi bilioni 2.5, kwa ajili ya mendeleo ya elimu, miundombinu na afya, hivyo madiwani wametakiwa kusaidia kukusanya mapato hayo ili asilimia fulani irudi kwenye kata zao kwa lengo la kuleta tija ya maendeleo kwa wilaya hiyo.

Naye, Mwenyekiti wa halmashauri wa Mbozi ambaye pia ni mwenyekiti wa mkutano huo Mheshimiwa Erick Ambakisye, amewasisitiza madiwani kutofumbia macho pindi wanapoona watendaji wa halmashauari kwa kushirikiana na mawakala hawakusanyi ushuru ipasavyo.

 Hata hivyo madiwani nao wamesema kutokana na makisio madogo wanayopewa na halmashauri wamekuwa hawatozi ushuru sahihi wa mazao, kwa magari yanayochukua mazao kutoka wilaya hiyo na kujinufaisha binafsi kwani kwa kufanya hivyo ni kuikosesha Serikali mapato.

Wakati huo huo bajeti hiyo ilisomwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Levison Chilewa, ambapo awali aliwasilisha bajeti ya bilioni 2.2 ambayo ilikataliwa na madiwani na kuongeza bilioni 2.2 hadi 2.5.

Wameongeza kuwa kuna vyanzo vingi vya mapato kama vile zao la kahawa, ufuta na mazao mchangantiko ya nafaka na biashara ambayo yanalimwa wilayani humo.

Mwenyekiti wa mkutano Bwana Erick aliwattuliza jazba madiwani baada ya diwani wa Kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka alipoinuka na kusema anawapongeza wananchi wa Arumeru kwa kumchagua mbunge wa CHADEMA, hali iliyopelekea Mwenyekiti wa mkutano kumkanusha kwa hapo wanajadili masuala ya maendeleo ya wilaya ya Mbozi na sio Jukwaa la siasa, mbona hakusema Lema alivyovuliwa ubunge, ambapo madiwani waliangua kicheko.

Mkutano huo ulimalizika kwa Mwenyekiti kuwataka madiwani kukutana Aprili 20 mwaka huu ili kujadili marekebisho ya bajeti hiyo.

 Mbali na upitishwaji wa bajeti hiyo, madiwani hao walimlaumu Mbunge wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde kwa kudhohofisha maendeleo katoka jimbo lake kutokana na kuwaambia wananchi wake wachangie shilingi  2,500 kwa ajili ya ujenzi wa shule ambazo hazitoshi kutokana na gharama za ujenzi kupanda.

Post a Comment

 
Top