Menu
 


Habari na mwandishi maalum.
Mawaziri saba wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa zao kwa kile kinachodaiwa ni shinikizo kutoka kwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambao unatokana na udhaifu katika utendaji wao wa kazi. 

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM, kilichoketi katika ukumbi wa Piusi Msekwa mara baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge usiku, waliojiuzulu ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi),GEORGE MKUCHIKA na Waziri wa Nishati na Madini, WILLIAM NGELEJA.

Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, EZEKIEL  MAIGE, Waziri wa Uchukuzi, OMARI NUNDU, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, HAJI MPONDA, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa JUMANNE MAGHEMBE na  Waziri wa Viwanda na Biashara, CYRIL CHAMI.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, MUSTAFA MKULO aliyetuhumiwa kuwa ni kiongozi wa ubadhirifu bungeni juzi na Mbunge wa Ludewa(CCM), DEO FILIKUNJOMBE, ameambiwa atafakari kwa sababu hayupo nchini. 

Chanzo hicho kilisema utendaji usioridhisha wa serikali ndio uliowafanya wabunge wa chama hicho kufikia hatua ya kushinikiza mawaziri hao wajiuzulu nyazifa zao.

Post a Comment

 
Top